Timu za Simba na Yanga mara nyingi zinapokutana huwa kuna mambo mengi ya kuchekesha huwa yanajitokeza, hususani utani wa mashabiki wa pande zote mbili kutoleana maneno ya utani kabla na baada ya mechi, hususani timu moja wapo inapomfung mwenzake.
October 1 2016 uwanja wa Taifa Dar es Salaam katika mchezo wa watani wa jadi uliochezwa na kumalizika kwa sare ya goli 1-1, Freeman Mbowe ambaye ni mbunge na kiongozi wa chama cha siasa cha CHADEMA alikuwa ni moja kati ya mashabiki waYanga waliojitokeza na kushangilia kwa furaha goli la Amissi Tambwe lililofungwa mkono ukiwa umehusika kucheza mpira.
Baada ya mechi mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ambaye ni shabiki wa Simbaalitumia account yake rasmi ya twitter na kuandika ujumbe wa utani kwa Freeman Mbowe ambaye alishangilia goli la utata la Tambwe “Mwenyekitiwangu Freeman Aikaeli Mbowe anatambua goli la mkono la Tambwe lakini hamtambui Lipumba “
No comments:
Post a Comment