Mgogoro wa Uongozi unaofukuta ndani ya Chama cha wananchi CUF unaendelea kuchukua sura Mpya baada ya kamati ya Uongozi ya chama hicho kutotambua mabadiliko ya kurugenzi ya chama hicho yaliyofanywa na M/kiti wa Cuf Prof Ibrahim lipumba ambaye alivuliwa madaraka na Baraza la Uongozi la Cuf hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm M/kiti wa kamati hiyo Julius Mtatiro amesema mabadiliko hayo hawayatambui huku pia wakishutumu msajili wa vyama vya siasa kwa kumtambua Prof.Lipumba kama m/kiti halali wa CUF kwa madai tayari wameshamvua uanachama.
Wabunge wa chama hicho wameomba kukutana na msajili wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.
No comments:
Post a Comment