Thursday, October 13, 2016

Chris Brown Hakuwa Kwenye Mood na Hakutaka Kuongea na Mtu – Vanessa Mdee


Mara nyingi wasanii wa nje wanapokuja kwenye show Afrika, hupenda kujichanganya na wasanii wanaotangulia kwenye show yake na kuchukua selfie na vitu kama hivyo. Lakini kwenye tamasha la Mombasa Rocks lililofanyika Oktaba 8 mjini Mombasa ambalo Chris Brown alitumbuiza, hakuna picha yeyote iliyoonekana akiwa na wasanii waliomsindikiza – Wizkid, Vanessa Mdee na Alikiba.

Kwa mujibu wa Vanessa, Chris hakuwa kabisa kwenye mood katika siku hiyo nzima na hakutaka kuongea na mtu. “To be honest, Breezy was not in a good mood,” Vanessa aliwaambia watangazaji wa XXL ya Clouds FM Jumatano hii.

“Tangia tumefika hadi tumeondoka hata ku.. sijui labda mazingira yalikuwa hayamfurahishi. Amepokelewa vizuri sana, sijui, alikuwa hana mood ya kusocialize na mtu yoyote,” ameongeza.

Kwa upande mwingine Vanessa alizungumzia sakala ya Alikiba kuzimiwa mic kwenye show hiyo.

“Mimi nilikuwa namsubiria Alikiba kama wewe ulivyokuwa unamsubiria, mimi nilikuwa nataka kuona show yake maana Mombasa wanamkubali sana but kilichotokea ni kwamba nadhani muda ulikuwa umeshatimia na Chis Brown muda wake wa kupanda stejini ulikuwa umeshafika, so that’s what happened, that’s what I know hayo mengine mimi siyajui,” alisisitiza.

“Halafu kibaya ni kwamba walikuwa wamesubiri kwa muda sana, kulikuwa na delay baada ya performance yangu mpaka alipopanda Wizkid, long time walikuwa wamesubiri na yeye [Chris Brown] alikuwa ameshaanza [kulalamika], ni kama nilivyosema alikuwa in a very bad mood. Kwahiyo walikuwa wanajaribu kumridhisha yeye ili apande muda ambao anataka yeye.”

No comments:

Post a Comment