Ligi Kuu England imepigwa leo michezo 7 katika ardhi ya England, tumeshuhudia baadhi ya timu zikichukua point zao tatu, wakati Man United wakiwa katika uwanja wao wa Old Trafford wameshinda kupata matokeo dhidi ya Burnley na kulazimishwa suluhu ya 0-0.
Kwa upande wa Arsenal wakiwa ugenini wamefanikiwa kuifunga Sunderland kwa jumla ya goli 4-1, Crystal Palace wakiwa kwao wamekubali kipigo cha goli 4-2 kutoka Liverpool, Tottenham Hotspurs wamewalazimisha Mabingwa watetezi wa EPL Leicester City sare ya 1-1, huku Man City wamefanikiwa kupata goli 4-0 dhidi ya West Bromwich huo unakuwa ushindi wao wa kwanza baada ya kushindwa kupata matokeo katika mechi zao sita zilizopita.
Magoli ya mechi ya Crystal Palace vs Liverpool, Full Time 2-4
Magoli ya mechi ya Sunderland vs Arsenal, Full Time 1-4
Magoli ya mechi ya Tottenham Hotspurs vs Leicester City, Full Time 1-1
Magoli ya mechi ya West Bromwich vs Man City, Full Time 0-4
No comments:
Post a Comment