Ndugu zangu,
Wakati tukisubiri mechi kubwa ya Watani Wa Jadi; Simba Vs Yanga' niwaletee simulizi elimishi za kandanda.
Mchezo wa kandanda ni sawa na sanaa, utamaduni. Ni siasa. Kwa wengine soka ni imani kama ilivyo imani nyingine za dini. Soka ni zaidi ya soka. Imejengeka kifalsafa.

Mathalan, katika Argentina kandanda ni sawa na dini kwa maana imani. Diego Maradona ni Mungu. Kuna wafuasi wa dhehebu la Maradona ndani na nje ya Argentina. Diego Armando Maradona ametokea kupendwa sana, na kuchukiwa sana pia.
Ni wanasoka wachache sana katika ulimwengu huu wa kandanda waliotokea kuibua hisia za wapenzi wa mchezo huo kwa namna ya pekee kama ilivyo kwa Maradona.
Uwezo wa Maradona katika ... Soma zaidi..
uchokozi wa kisoka na umahiri wake katika kulisakata kandanda ulionekana bayana mwaka ule wa 1986.
Ni katika michuano ya Kombe la Dunia, na hususan katika pambano la Argentina dhidi ya Uingereza.
Kwanza Maradona alifunga goli la mkono, baadae kidogo Maradona alifunga goli la kiufundi na kibingwa pale alipoambaa kwa kasi na mpira akitokea nusu ya uwanja. Aliwapiga chenga za maudhi karibu wachezaji wote wa Uingereza waliomkabili. Kisha aliukwamisha mpira kimiani.
Maradona alidhihirisha umahiri wake katika sanaa ya kandanda. Itakumbukwa , Argentina ilishinda Kombe la Dunia mwaka ule.
Miaka minne baadae, juhudi za Maradona binafsi ziliiwezesha nchi yake kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Dunia. Katika fainali zile mechi kati ya Brazil na Argentina ndiyo iliyokuwa na kivutio cha pekee.
Brazil waliwazidi Argentina katika idara zote uwanjani, hivyo basi, Argentina na Maradona hawakupumua kwa muda mrefu wa mchezo. Lakini, mara, na kama radi, alizinduka Diego Maradona. Akiwa amenabwa vikali na walinzi wa Brazil, Maradona
alifanikiwa kutoa pasi muhimu kwa Claudio Caniggia aliyefunga goli pekee katika mchezo huo.
Argentina waliingia fainali na kushindwa na Ujerumani. Fainali za Kombe la Dunia za 1994 zilimshuhudia Maradona akiwa katika hatua za kuporomoka kisoka. Alijitahidi kidogo katika mechi za awali, kisha likalipuka bomu. Maradona alibainika kutumia vidonge vya kuongeza nguvu aina ya efedrin. Argentina nayo ikapotoea katika hatua za awali za fainali hizo.
Naam, Soka kama dini ina wafuasi wengi. Mpira ule wa mviringo,
wenye kudunda ni kama Mungu wa soka. Bila mpira uwanjani hakuna soka. Kama ulivyo mpira wenyewe, mviringo, wenye sura nyingi na wenye kudunda, basi,hata pambano lenyewe la soka laweza kuwa na sura nyingi.
Naam. Mpira unadunda, katika soka lolote laweza kutokea.
Soka, kandanda, kabumbu, kipute au ndinga. Yote hayo na mengineyo ni majina yenye kuzungumzia aina moja ya mchezo; mpira wa miguu. Kuna aina nyingi za michezo ya mipira; kuna mpira wa wavu, mikono, meza, pete na mingineyo.
Michezo yote hiyo niliyoitaja hapo juu inatofautina sana na mchezo
wa mpira wa miguu. Ni kwanini basi michezo hiyo na mingine yenye kuhusisha mpira isiwe na wapenzi wengi kulinganisha na mpira wa miguu? Jibu lake linapatikana kwa kutafakari falsafa nzima ya kandanda.
Kandanda huchezwa kwa kutumia miguu. Hii ndio inatufanya wengi tuvutiwe na mchezo huu. Kupitia kandanda tunaona kuwa binadamu anaweza kufanya mambo mengi ya ajabu kwa kutumia mguu wake. Ni mambo yenye kutoa burudani kwa anayetazama. Ndio maana hatuchoki kushabikia mchezo huu.
Kama lilivyo jina la mchezo wenyewe, yaani mpira wa miguu, basi,
mchezaji haruhusiwi kutumia mikono. Ni golikipa tu anayerusiwa kutumia mikono katika kuudaka mpira uliopigwa kwa mguu. Golikipa amepewa eneo lake dogo la kujidai kwa kutumia mikono yake. Nje ya eneo hilo golikipa naye haruhusiwi kutumia mikono, bali miguu.
Mpira unatakiwa wakati wote huwe ndani ya uwanja. Mpira unaotoka nje unaweza kurushwa kwa mikono kuingizwa uwanjani, aliye uwanjani haruhusiwi kuupokea kwa mikono isipokuwa golikipa.
Katika mpira wa miguu mchezaji anaruhusiwa kutumia sehemu
nyingine zote za mwili, kichwa, kifua, tumbo, mgongo, kisigino na hata kidevu, lakini , kamwe si mkono. Dhambi kubwa katika soka ni kwa mchezaji kuucheza mchezo huo kwa kutumia mkono, na kibaya zaidi akifanya hivyo kwa kudhamiria, kwa makusudi. Dhambi hiyo haisameheki katika soka, adhabu yake ni kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Mkono ni shetani wa soka.
Waingereza ambao kihistoria ndio waliovumbua mchezo wa soka mwaka 1908, kamwe hawatakoma kumlaani Diego Maradona wa Argentina kwa kufunga goli la mkono nililolielezea hapo juu. Kwa Waingereza, Maradona alifunga goli kwa kumtumia shetani wa soka. Maradona mwenyewe anadai ni mkono wa Mungu!
Mpira wa miguu umechangia katika kuleta furaha kwa mamilioni ya
watu hapa ulimwenguni, pale timu ama taifa linaposhinda mashindano muhimu. Lakini mchezo huu umekuwa pia ni chanzo cha huzuni kwa mamilioni ya watu katika ulimwengu huu, pale timu au taifa linaposhindwa katika mashindano muhimu.
Mpira wa miguu unaingia katika historia ya Dunia kwa kuwa chanzo cha vita baina ya mataifa. Katika mika ya sabini, kule Marekani ya Kusini, nchi za El Salvador na Honduras zilingia vitani kutokana na matokeo ya mpira wa miguu baina ya timu za nchi hizo mbili! Mpira ni siasa pia, kuna serikali au viongozi waliobaki ama kuondoka madarakani kutokana na matokeo ya mechi za mpira wa miguu.
Siku moja nitawasimulia kisa kile cha mataifa yaliyoingia vitani kwa matokeo ya uwanjani.
Nawatakia burudani njema ya soka jioni ya leo.
Maggid,

No comments:
Post a Comment