Sunday, October 16, 2016

Assist ya Samatta imeinusuru KRC Genk na kipigo cha tano msimu huu

Baada ya watanzania kupokea good news ya nahodha wao wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta kuteuliwa katika list ya majina 30 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika 2016, nyota huyo usiku wa October 15 alishuka dimbani kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuwania point tatu ugenini dhidi ya Mouscron.

Samatta ambaye alianzia benchi na kuingia kipindi cha pili dakika ya 67 kuchukua nafasi ya mjamaica Leon Bailey, alishuhudia timu yake ya KRC Genk ikiwa nyuma kwa goli 2-1 hadi alipoingia kwenda kuongeza nguvu dakika ya 78 akafanikiwa kutoa assist na kuinusuru KRC Genk isipoteze mchezo wa tano wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu huu.

No comments:

Post a Comment