Tuesday, October 25, 2016

Huyu ndio CEO wa Yanga kutoka Ufaransa

Ukiachana na headlines za uongozi wa klabu ya Yanga kudaiwa kumleta kocha mpya katika klabu hiyo George Lwandamina kutoka Zesco United ya Zambia taarifa mpya zimetoka Yanga wamemteua mfaransa Jerome Dufourg kuwa afisa mtendaji mkuu wao(CEO).

Yanga wameripotiwa kumpa nafasi hiyo Jerome Dufourg ambaye ni mtaalam wa sports business kufuatia mwenyekiti wao Yusuph Manji kudai kuwa Yanga ilipata hasara ya zaidi ya Tsh bilioni 1.5 kwa mwaka jana, Dufourg anatajwa kupewa majukumu ya kuendesha shughuli za klabu hiyo na mipango ya fedha.
dcea
Muda wowote kutokea sasa Jerome Dufourg atawasili Tanzania lakini kazi ataanza rasmi November 19 2016, Dufourg amewahi kufanya kazi na shirikisho la soka laRwanda pamoja na klabu ya FC Talanta ya Ligi daraja la kwanza Kenya, chanzo cha taarifa hizi ni @shaffihdauda na twitter account ya @JeromeJDufourg

No comments:

Post a Comment