Thursday, October 13, 2016

MAANDAMANO NCHINI COLOMBIA

Juan Manuel Santos
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos(katikati) akiwa ameshika nakala ya makubaliano ya amani na Waasi wa FARC
Maelfu ya watu wanaandamana katika miji kadhaa nchini Colombia ili kushinikiza kuzingatiwa kwa makubaliano yaliyosainiwa na serikali na waasi wa FARC.
Huko Bogota familia za wahanga wa mgogoro kati ya waasi hao na serikali walipewa maua meupe kama ishara ya amani.

Makubaliano hayo yamekuja baada ya muda mrefu wa mazungumzo lakini mapema mwezi huu watu wengi walipinga makubaliano hayo katika kura ya maoni.
Kiongozi wa FARC Timochenko amesema kuwa atasita kujadili tena moja ya kifungu tata ambacho kinahusu kupunguzwa kwa adhabu ya kifungo kwa watakaokubali kuwa walikiuka haki za binadamu. BBC

No comments:

Post a Comment