Saturday, October 29, 2016

AZAM FC... TUTAPELEKA MAUMIVU TENA LEO KWA KAGERA SUGAR,POINTI TATU MUHIMU KWETU

Image result for Azam FC
Na.jom_thefuture
Timu ya Azam FC inatarajia kutupa karata yake ya kwanza muhimu kwa kucheza na Kagera Sugar Leo mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara utakaopigwa uwanja wa Kaitaba huku Kocha Mkuu Zeben Hernandez ametamba kuwa watakuwa na kazi moja tu ya kusaka alama tatu katika kipute hicho.

Akizungumza amesema kuwa ni mechi nzuri tunayotakiwa kuzoa pointi tatu, hali ya timu haipo vizuri sana kutokana na matokeo, lakini nafikiria kuwa mechi ya mwisho tuliyocheza na kupata ushindi ilibadilisha mawazo ya wachezaji.
“Malengo yetu ni kuendelea kuboresha kiwango cha timu na kushinda pointi tatu kesho, kwa sababu nafikiria kuwa mashabiki, wachezaji na Azam FC kwa ujumla wanahitaji pointi tatu,” alisema Hernandez.
Kocha huyo wa zamani wa Santa Ursula ya Hispania, aliweka wazi kuwa katika mchezo huo atawakosa nyota wake watatu ambao ni mabeki Shomari Kapombe, Bruce Kangwa na kiungo Himid Mao, aliyepata kadi nyekundu kwenye mchezo uliopita dhidi ya JKT Ruvu.
Azam FC itaingia kwenye mchezo huo, ikiwa inakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16, hivyo ushindi wowote wa Leo utaifanya kufikisha jumla ya pointi 19 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya nne ikizishusha Mtibwa Sugar (17) na wapinzani wao hao Kagera (18).(P.T)

No comments:

Post a Comment