Burudani ya michezo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliendelea usiku wa October 18 2016 kwa viwanja 8 kuchezwa michezo 8 ya hatua ya makundi round ya tatu, moja kati ya michezo iliyoshuhudiwa ikimalizika kwa idadi kubwa ya magoli ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Legia Warszawa mchezo uliochezwa katika dimba la Santiago Bernabeu.
Real Madrid ambao ndio Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya UEFA Champions League wamedhihirisha kwa mara nyinine ubora wao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kumuadhibu Legia Warszawa kwa goli 5-1, magoli ya Real Madridyalifungwa na Gareth Bale dakika ya 16, Tomasz Jodlowiec aliyejifunga dakika ya 20.
Dakika ya 22 Legia walifanikiwa kupata goli lao na kwanza na pekee kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Miroslav Radovic, kabla ya dakika ya 37 Marco Asensio kuifungiaReal Madrid goli la tatu, Lucas Vazquez alipachika goli la nne dakika ya 68 na Alvaro Morata akapachika goli la tano dakika 84.
Ushindi huo umeifanya Real Madrid kushika nafasi ya pili katika kundi lao linaoongozwa na Borussia Dortmund wenye point 7 sawa na wao wakipishana kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
No comments:
Post a Comment