Thursday, October 27, 2016

Mourinho kalipa kisasi kwa Guardiola

September 10 2016 ilikuwa siku ya kihistoria kwa makocha waliokuwa na upinzani tokea wakiwa katika Ligi Kuu Hispania Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakati huo walikuwa wanakutana kwa mara ya kwanza wakiwa wanafundisha vilabu pinzani vya Ligi Kuu England Man United na Man City.

Siku hiyo ikiwa ndio ya kwanza kukutana kwa Mourinho na Guardiola wakiwa katika Ligi Kuu England, ulimwengu ulishuhudia Man United ya Jose Mourinho ikifungwa na Man City ya Pep Guardiola kwa magoli 2-1, magoli yaliofungwa na Kelvin De Bruyne dakika ya 15 na Kelechi Iheanacho.
39bf2e7700000578-3875938-image-a-63_1477513835668
Sasa usiku wa October 26 wapinzani hao wakakutana tena katika mchezo wa EFL Cup wakiwa katika dimba la Old Trafford, Man United ilifanikiwa kuifunga Man City kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Juan Mata dakika ya 54 na kuufanya mchezo umalizike kwa Jose Mourinho kulipa kisasi cha September 10 2016.

No comments:

Post a Comment