Saturday, September 24, 2016

Nay wa Mitego Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Toka Shamsa Ford Kuelewa na Mwanaume Mwingine...Adai Alimwambia Anaenda Kuolewa


Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Nay Wa Mitego amesema Shamsa ni ‘wife material’ hivyo anamtabiria kudumu katika ndoa yake.

“Ndoa ni kitu cha heri lakini sometime watu wanaweza wakaoana kwa kutafuta experience za ndoa zinakuwaje, watu wakioana inakuwaje, ukishapata experience kila mtu anaendelea kupuyanga,” alisema Nay. “Sasa mimi sijajua kama wao wanatafuta experience za ndoa ili kujua watu wakioana wanakuwaje,”

Aliongez, “Kwa jinsi ninavyomjua Shamsa ni mwanamke kweli, kwa sababu ni mwanamke ambaye anastahili kuwa mke kwa sababu amekaa ‘kiwife material’ kiukweli kabisa, sijui mtu ambaye ameenda kuolewa naye na kuna vitu yeye mwenyewe anatakiwa kubadilika,”

Rapper huyo amedai Shamsa kabla hajaolewa alimwambia kwamba anaenda kuolewa na akampatia baraka zote.

No comments:

Post a Comment