![](https://scontent-lhr3-1.xx.fbcdn.net/v/t1.0-9/14440694_10209167481436897_1988142850888034052_n.jpg?oh=83776b0768fc13460fdee73ea72691f4&oe=5864CDC1)
Akiongea na waandishi wa habari ofisi kuu ya CUF Buguruni Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba ameuita mkutano wa CUF uliofanyika Zanzibar kama ''kikao cha harusi'' kwani haukufuata katiba, alitoa hoja zifuatazo;
Anamtaka Maalim Seif aje Dar kumletea taarifa za utendaji wa chama kwani yeye ndiye mwenyekiti halali.
Anamtaka Maalim Seif aje Dar kumletea taarifa za utendaji wa chama kwani yeye ndiye mwenyekiti halali.
Amesema 'ni mkutano mkuu tu kwa mujibu wa katiba ya CUF kifungu 72(2)a wenye mamlaka ya kumuonya au kumfukuza Mwenyekiti na sio baraza la uongozi.
Pia alieleza kikao hicho hakikukidhi sharia kwani kilihudhuriwa na wajumbe watatu tu kutoka bara ambao ni wajumbe wa kamati kuu huku katiba ikitaka wahudhurie wajumbe 22 wa kamati kuu.
Source: Daily News 29.09.2016.
Nyongeza ya Mtanzania 29.9.2016
Kauli ya Lipumba
Kauli ya Lipumba
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema atampokea Maalim Seif siku yoyote atakayofika na pamoja na mambo mengine atapanga naye mikakati ya ujenzi wa chama.
Alisema CUF inamtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu, hivyo basi hawezi kumtenga atakapofika kwenye ofisi hizo zilizopo Buguruni kwa sababu kuna ofisi yake ya kufanyia kazi.
“Namsubiri Maalim Seif aje kwenye ofisi zetu za Buguruni ili tukae na kukijenge chama kwa sababu anatambua kuwa mimi ni mwenyekiti halali kwa mujibu wa soma zaidi..
Katiba yetu. Kinachojitokeza sasa ni migongano ya siasa ambayo inaweza kumalizika wakati wowote.
“Naamini siku atakayokuja tutampokea na kumpeleka ofisini kwake kwa ajili ya kuchapa kazi, lakini pia nitampa mwongozo wa namna ya kukijenga chama ikiwa ni pamoja na kumwambia kuwa fedha zisitutenganishe,”alisema Prof. Lipumba.
Akizungumzia kikao cha Baraza Kuu kilichofanyika Visiwani Zanzibar ambacho pamoja na mambo mengi kilitangaza kumvua uanachama, a alisema kikao hicho ni batili na kimekiuka katiba ya chama hicho.
Alisema kikao chenye wajibu wa kumfukuza uanachama ni Mkutano Mkuu pekee ambao unawashirikisha wajumbe wote kutoka kila upande wa Bara na Zanzibar.
“Kifungu cha 79(2)(a) cha Katiba ya chama hicho kinasema kuwa, Mkutano Mkuu unaweza kuchukua hatua za nidhamu zozote zile zikiwamo kumuachisha au kumfukuza uongozi au uanachama au yote mawili, mwenyekiti wa chama hicho.
“Mimi navuliwa uanachama na Mkutano Mkuu, siyo baraza la uongozi ambalo na lenyewe halijakidhi matakwa ya katiba ya chama... kilichofanyika Zanzibar ni sawa na kikao cha harusi,” alisema.
Alisema licha ya kufanyika kikao hicho, pia idadi ya wajumbe waliohudhuria kutoka upande wa bara ni tisa kati ya 22 na wajumbe watatu ni wakurugenzi huku wanachama wa kawaida walikuwa sita.
Profesa Lipumba alisema kwa mujibu wa Katiba ya CUF, kikao cha Baraza Kuu huitishwa na mwenyekiti na hutakiwa kukutana kila baada ya miezi minne isipokuwa kama kuna dharura. Linakutana chini ya mwenyekiti na si vinginevyo, alisisitiza.
“Kifungu cha 83(1) ambacho kinalipa mamlaka Baraza Kuu kuwasimamisha uongozi na siyo kuwavua uanachama viongozi wakuu wa chama ambao ni Mwenyekiti, Makamu na Katibu Mkuu. Hivyo baraza halina uwezo wa kunivua uanachama,” alisema.
Alisema katiba hiyo, kifungu cha 83(5) kinasema, baraza hilo linaweza kuchukua hatua za nidhamu ikiwa ni pamoja na kutoa onyo kwa maandishi na karipio kali.
Alisema hakuna hatua zilizofuatwa katika Baraza Kuu hasa kwa kumvua uanachama ila kuna fitina zinazochochewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).
“Mimi sifukuziki ndani ya chama hiki, wala sisusi, nimelipia kadi yangu hadi mwaka 2020, nitaendelea kukipigania chama hiki hadi mwisho, sihami, siondoki...wala siendi mahakamani, nipo ngangari, wakija Buguruni watanikuta kama mwenyekiti wa chama,” alisema.
Juzi, Baraza Kuu la Uongozi la CUF lilitangaza kumvua uanachama Profesa Lipumba kwa kile kilichoelezwa kukaidi wito wa kwenda kujieleza kwa kuvamia ofisi za CUF za Buguruni na kufanya uharibifu wa mali za chama.
Septemba 23, Msajili wa vyama Jaji, Francis Mutungi, alimrejesha katika nafasi yake ya uenyekiti na siku iliyofuta kiongozi huyo alikwenda ofisini kwake Buguruni na kuzuka tafrani hiyo.
No comments:
Post a Comment