Tuesday, September 13, 2016

Mesen Selekta adai yeye ndiye Producer pekee anayetengeneza muziki wa Singeli.



Producer Mesen Selekta kutoka Defatality studio’s amefunguka na kusema kuwa yeye ndiye producer pekee anayetengeneza muziki halisi wa Singeli.

Akiongea kwenye kipindi cha The Base cha ITV,Mesen amedai kuwa ma producer wengi wanajaribu kutengeneza singeli lakini wanakosea kwa kufananisha muziki huo na mnanda.
Unajua kuna muziki unaitwa singeli,kuna mnanda na ladha,sometimes kuna baadhi ya producer wanajaribu kutengeneza singeli lakini inakuwa sio singeli unakuwa una sound kama mnanda au ladha na ndio maana mpaka sasa hivi Mesen anabaki kuwa producer pekee wa Singeli” alifunguka Mesen.


No comments:

Post a Comment