Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.
Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.
Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-
= TBL Wamechangia Milioni 100
= Azania Group Wanatanguliza Milioni 20
= Wafanyabiashara wa Mafuta wa rejareja watakusanya Milioni 250 na watakabidhi ijumaa ya week hii
= Kagera Sugar wanatoa Milioni 100 na tani 10 za sukari.
= Serengeti wanatoa saruji mifuko 800
= Pepsi Cola 50 Millioni
= Hatiamaye Regnald Mengi anatoa mchango wake wa Milioni 110.
= Protas Ishengoma anatoa msaada wa Milioni 5.
= GBP, MOIL na OILCOM wameahidi kujenga shule mbili (Ihungo na Nyakato) zilizoharibiwa vibaya.
= Puma wanachangia 50 Milioni
= Agusta Tanzania wanatoa Milioni 10
= Camel Oil wanachangia mifuko 1,000 ya Cement
= Tippa waachangia milioni 20
= Orexy wanachangia Milioni 50
= Waislamu wa madhehebu ya Al-Shafy, Ijumaa na Adhuhuri wanachangia Milioni 1.
= Sahara Tanzania wanachangia Milioni 20
Wizara ya Mambo ya Nje watafanya matembezi ili kuhamashisha uchangishaji wa fedha na wataanzia Polisi Oysterbay.
MAJUMUISHO:
Waziri Charles Mwijage nafanya majumuisho ya fedha zilizopatikana ni kama ifuatavyo:
1. Fedha taslimu ni Milioni 646,
2. Ahadi ni Milioni 705,
3. Dola za Kimarekani 10,000
4. Yuro 10,000.
5. Mfuko ya Sementi zaidi ya 2800,
6. Ahadi ya ujenzi wa Shule mbili ndani ya siku 30.
JUMLA KUU, Bilioni 1 na Na Zaidi ya Milioni 300
======
Ahsanteni kwa kuwa nami........
No comments:
Post a Comment