Wednesday, September 14, 2016

Master J Aliniambia Sijui Kuimba – Harmonize

Mkali wa wimbo ‘Bado’ Harmonize amefunguka na kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafika kwenye mafanikio huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindalo la BSS.

Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.
“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”
Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.
“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”
Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.

No comments:

Post a Comment