September 9 2016 Kalapina wa kikosi cha mizinga ambaye pia amekua akifanya TV show yenye harakati za kuokoa Watanzania kwenye utumiaji wa dawa za kulevya, alisema amesikia lakini hana uhakika kuhusu ishu ya Chidi Benz kurudi kutumia dawa za kulevya.
Ikumbukwe kwamba Kalapina na meneja wa WCB Babu Tale ndio walihusika kumpeleka rapper Chidi Benz kwenda kwenye nyumba ya matibabu Bagamoyo ili aachae na utumiaji wa dawa za kulevya ambazo alikiri kuzitumia.
Sasa millardayo.com imempata Chidi Benz na kumpa nafasi aseme kama ni kweli stori zilizosambaa kwamba amerudi tena kwenye utumiaji wa dawa za kulevya na majibu yake ni haya hapa chini.
‘Nashukuru sana kwasababu kuna kitu nilikuwa nataka kusema ila uongozi wangu ulinikataza kuongelea hiyo ishu, nimesikia taarifa kwamba jamaa fulani huwa anaongea masuala flani yale ambayo niliyowahi kuzungumziwa katika media mbalimbali’
‘Ningependa kusema hivi asipende kutengeneza stori flani kuhusu mimi bali kama aliamua kuandaa kipindi na kuwasaidia watu wanaojihusisha na dawa aendele lakini sio kupitia mimi kwani naweza kuchukua uamuzi wowote labda nikaamua kwenda kufungua kesi Mahakamani kwani amenitangazia mabaya habari ambazo si za kweli’
Unataka kumsikiliza Chidi Benz mwenyewe akiiongelea hii? bonyeza play hapa chini
No comments:
Post a Comment