Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa kwanza waEuropa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku wa Septemba 29 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi A Europa Leaguedhidi ya Zorya.
Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Feyenoordambao walikuwa na rekodi ya kushinda mechi nane mfululizo, wamecheza mchezo wao wa pili wa Europa League dhidi ya Zorya katika uwanja wao wa Old Trafford na kufanikiwa kushinda kwa goli 1-0 lililofungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 69.
Kufuatia ushindi huo Man United wanakuwa nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi A linaloongozwa na Fenerbahce aliyepata ushindi wa kwanza wa Europa League leo dhidi ya Feyenoord na kuivunjia rekodi yao ya kucheza mechi 9 bila kufungwa, nafasi ya pili wakiwa Feyenoord na Zorya wakishika mkia kwa kusalia na point moja, Man Unitedwatacheza mchezo wao wa tatu dhidi ya Fenerbahce October 20 2016.
No comments:
Post a Comment