Usiku wa Septemba 24 2016 jiji la London lilikuwa busy kwa upande wa mashabiki wa soka kwani mashabiki wa timu kubwa za Arsenal na Chelsea walikuwa busy kufuatilia mchezo dhidi ya vilabu vyao ambavyo vyote vinatokea ndani ya jiji la London.
Mchezo kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea ulichezwa katika dimba la Emirates, tofauti na ilivyozoeleka rekodi ya Arsenal ya mechi 9 mfululizo kucheza dhidi ya Chelsea kushindwa kuibuka na ushindi wowote na kuishia kutoa sare tatu na kati ya mechi hizo 9 alikuwa karuhusu kufungwa nyumbani mechi 2 na sare 3.
Hata hivyo rekodi za jumla zinaonesha Arsenal amewahi kumfunga Chelsea mara 73 na kuwahi kufungwa mara 61, wakiwa wamewahi kusuluhu mechi 54, mchezo wa Septemba 24 Arsenal wameutumia kurudisha heshima yao na kuifunga Chelsea kwa goli 3-0, magoli ambayo yalifungwa na Alexis Sanchez dakika ya 11, Theo Walcott dakika ya 14 na Mesut Ozil dakika ya 40.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0
No comments:
Post a Comment