Mourinho alijiridhisha kuwa mwamuzi Clattenburg alitakiwa kumtoa kipa Claudio Bravo kwa kadi nyekundu na kuipa Manchester United penalti baada ya kipa huyo wa Manchester City kumchezea vibaya Wayne Rooney kipindi cha pili, huku pia mwamuzi akikataa kuipa Manchester United penalti nyingine wakidai Nicolas Otamendi alinawa mpira. “Tumeumizwa na Mark kwa uamuzi wake mbaya wa kipindi cha pili,” alisema Mourinho. “Najua sheria za mchezo huu. Bila ubishi ile ilikuwa penalti na kadi nyekundu kwa Bravo. Kama ni nje ya eneo la hatari, ingekuwa ni mkwaju wa adhabu na kadi nyekundu. “Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2 muda mrefu, lakini kwa sasa tunazungumza kitu kingine.” Mourinho pia aliwashukia baadhi ya wachezaji wake Jesse Lingard, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba akidai kuwa walikuwa wakicheza kwa uwezo binafsi zaidi na kukataa kufuata maelekezo yake. “Niliwaambia walipokuwa mapumziko kuwa baadhi yao wanajaribu kufanya mambo ambayo niliwakataza, walikuwa wakicheza kwa uwezo binafsi zaidi,” aliongeza kocha huyo wa Ureno. Install SIASA HURU App Kwenye Simu Yako Kusoma Habari hizi Kirahisi, Bonyeza HAPA
Tuesday, September 13, 2016
Jose Mourinho Amshukia Mwamuzi Baada ya Kichapo Cha Man City

Labels:
michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment