Usiku wa Septemba 13 2016 michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ilianza rasmi kwa michezo nane kupigwa katika ardhi ya bara la Ulaya, kwa upande wa Arsenalwalicheza dhidi ya klabu ya Paris Sait Germain ya Ufaransa katika uwanja wa Parc des Princes jijini Paris Ufaransa.
Arsenal waliingia katika ardhi ya Ufaransa wakiwa na rekodi ya kucheza na timu zaUfaransa mara 18, kufanikiwa kuibuka na ushindi mara 11 sare 4 na kupoteza michezo mitatu, wamefanikiwa kutoka sare ya goli 1-1, awali mchezo ulianza kwa PSG kufunga goli dakika ya kwanza kupitia kwa Edinson Cavani, na kuendelea kulishambulia lango laArsenal ila golikipa David Ospina alifanikiwa kuokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa PSG.
Licha ya PSG kumiliki mpira kwa asilimia 55 kwa 45 kwa kipindi chote cha mchezo,Arsenal walifanikiwa kusawazisha goli dakika ya 78 kupitia staa wake wa kimataifa wa Chile Alexis Sanchez, kufuatia suluhu hiyo Arsenal wanakuwa wamerudia rekodi yao ya March 29 1994 dhidi ya PSG ambapo mchezo wao wa UEFA European Cup Winners Cup ulimalizika kwa sare ya goli 1-1.
No comments:
Post a Comment