Kiungo wa kimataifa wa Armenia aliyejiunga na Man United msimu huu akitokeaBorussia Dortmund ya Ujerumani Henrikh Mkhitaryan amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu kutopata nafasi ya kutosha kuitumikia Man United.
Mkhitaryan amefunguka wakati alipoteuliwa kuwa balozi wa UNICEF kwa nchi yake yaArmenia, kuwa kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha Man Unitedhakuvunji ndoto zake za kuendelea kuitumikia Man United.
“Ni kweli nimekuwa nikipata nafasi ndogo ya kucheza Man United lakini sitokata tamaa, ilichukua muda mrefu kupata nafasi ya kujiunga na Man United, hivyo hakuna kitakachonizuia kutimiza ndoto zangu”
Mkhitaryan alijiunga Man United mwaka huu katika dirisha kubwa la usajli kwa dau la pound milioni 26 akitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani, lakini amekuwa hapati nafasi kubwa ya kucheza chini ya Jose Mourinho.
No comments:
Post a Comment