Wednesday, November 9, 2016

Inawezekana Sanchez akawa nje ya uwanja kufuatia taarifa hizi By Rama Mwelondo TZA


Staa wa Arsenal Alex Sanchez aliungana na wachezaji wenzake wa timu ya yao ya taifa ya Chile jana November 7 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia 2018  dhidi ya Colombia.

Taarifa zilizoripotiwa leo Jumanne ya November 8 2016 kuhusu staa huyo ni kuwa amepata majeruhi wakati wa mazoezi ya pamoja na wenzake, Sanchez mwenye umri wa miaka 27 alishindwa kuendelea mazoezi baada ya kupata majeruhi.
alexis-sanchez
Sanchez amefanyiwa uchunguzi na wataalam wa afya wa timu ya taifa ya Chile na inasubiria taarifa ya mwisho kama ataweza kucheza mchezo dhidi ya ColombiaNovember 10 2016 au la.

No comments:

Post a Comment